5. Maana kabla ya mavuno, maua yaangukapo, na maua yakawa zabibu zianzazo kuiva, ndipo atakapoyakata matawi kwa miundu, na kuviondoa vitawi vilivyopanuka na kuvikata.
6. Wote pamoja wataachiwa ndege wakali wa milimani, na hayawani wa nchi; ndege wakali watakaa juu yao wakati wa jua, na hayawani wote wa nchi watakaa juu yao wakati wa baridi.
7. Wakati huo BWANA wa majeshi ataletewa hedaya na watu warefu, laini;Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa;Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu,Ambao mito inakata nchi yao;Mpaka mahali pa jina la BWANA wa majeshi, mlima Sayuni.