1. Ufunuo juu ya Dameski. Tazama, Dameski umeondolewa usiwe mji, nao utakuwa chungu ya magofu.
2. Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa kwa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu.
3. Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi.