Isa. 14:3-10 Swahili Union Version (SUV)

3. Tena itakuwa katika siku ile, ambayo BWANA atakupa raha baada ya huzuni yako, na baada ya taabu yako, na baada ya utumishi ule mgumu uliotumikishwa;

4. utatunga mithali hii juu ya mfalme wa Babeli, na kusema,Jinsi alivyokoma mwenye kuonea;Jinsi ulivyokoma mji ule wenye jeuri!

5. BWANA amelivunja gongo la wabaya,Fimbo ya enzi yao wenye kutawala.

6. Yeye aliyewapiga mataifa kwa ghadhabu,Kwa mapigo yasiyokoma;Aliyewatawala mataifa kwa hasira,Ameadhibiwa asizuie mtu.

7. Dunia yote inastarehe na kutulia;Hata huanzilisha kuimba.

8. Naam, misunobari inakufurahia,Na mierezi ya Lebanoni, ikisema,Tokea wakati ulipolazwa chini wewe,Hapana mkata miti aliyetujia.

9. Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako,Ili kukulaki utakapokuja;Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako,Naam, walio wakuu wote wa dunia;Huwainua wafalme wote wa mataifa,Watoke katika viti vyao vya enzi.

10. Hao wote watajibu na kukuambia,Je! Wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi!Wewe nawe umekuwa kama sisi!

Isa. 14