21. Fanyeni tayari machinjo kwa watoto wake.Kwa sababu ya uovu wa baba zao;Wasije wakainuka na kuitamalaki nchi,Na kuujaza miji uso wa ulimwengu.
22. Nami nitainuka, nishindane nao; asema BWANA wa majeshi; na katika Babeli nitang’oa jina na mabaki, mwana na mjukuu; asema BWANA.
23. Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema BWANA wa majeshi.
24. BWANA wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea;
25. kwamba nitamvunja huyo Mwashuri vipande vipande katika nchi yangu, na juu ya mlima wangu nitamkanyaga chini ya miguu yangu; ndipo nira yake iliyo juu yao itakapoondoka, na mzigo wake utatoka mabegani mwao.
26. Hilo ndilo kusudi lililokusudiwa duniani mwote, na huo ndio mkono ulionyoshwa juu ya mataifa yote.