Hes. 7:31-34 Swahili Union Version (SUV)

31. matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

32. na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

33. na ng’ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

34. na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

Hes. 7