Hes. 6:22-27 Swahili Union Version (SUV)

22. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

23. Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia;

24. BWANA akubarikie, na kukulinda;

25. BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili;

26. BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.

27. Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia.

Hes. 6