39. Naye Haruni alikuwa mtu wa umri wa miaka mia na ishirini na mitatu hapo alipokufa katika mlima wa Hori.
40. Ndipo Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyekaa pande za Negebu katika nchi ya Kanaani akasikia habari za kuja kwao wana wa Israeli.
41. Nao wakasafiri kutoka mlima wa Hori, wakapanga Salmona.
42. Wakasafiri kutoka Salmona, wakapanga Punoni.
43. Wakasafiri kutoka Punoni, wakapanga Obothi.
44. Wakasafiri kutoka Obothi, wakapanga Iye-abarimu, katika mpaka wa Moabu.
45. Wakasafiri kutoka Iye-abarimu, wakapanga Dibon-gadi.
46. Wakasafiri kutoka Dibon-gadi, wakapanga Almon-diblathaimu.
47. Wakasafiri kutoka Almon-diblathaimu, wakapanga katika milima ya Abarimu, kukabili Nebo.
48. Wakasafiri kutoka hiyo milima ya Abarimu, wakapanga katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko.
49. Wakapanga karibu na Yordani, tangu Beth-yeshimothi hata kufikilia Abel-shitimu katika nchi tambarare za Moabu.
50. Kisha BWANA akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko, na kumwambia,
51. Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani,
52. ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunja-vunja mahali pao pote palipoinuka;