Hes. 32:40-42 Swahili Union Version (SUV)

40. Basi Musa akampa Makiri, mwana wa Manase, Gileadi, naye akakaa humo.

41. Kisha Yairi mwana wa Manase akaenda na kuvitwaa vijiji vya Gileadi. Akaviita jina lake Hawoth-yairi.

42. Kisha Noba akaenda na kutwaa Kenathi na vijiji vyake, na kuita jina lake Noba, kwa kuandama jina lake mwenyewe.

Hes. 32