Hes. 29:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Tena mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; ni siku ya kupiga tarumbeta kwenu.

2. Nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng’ombe mume mdogo mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba;

3. pamoja na sadaka yake ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa ng’ombe, sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume,

Hes. 29