28. pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa kila ng’ombe, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume,
29. na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo, wa wale wana-kondoo saba;
30. na mbuzi mume mmoja, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
31. Zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, mtasongeza wanyama hao (watakuwa wakamilifu kwenu), pamoja na sadaka zake za vinywaji.