26. Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli.
27. Hizi ndizo jamaa za Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, sitini elfu na mia tano.
28. Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu.
29. Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi.
30. Hawa ndio wana wa Gileadi; wa Abiezeri, jamaa ya Waabiezeri; wa Heleki, jamaa ya Waheleki;