Hes. 26:15-20 Swahili Union Version (SUV)

15. Na wana wa Gadi kwa jamaa zao; wa Sifoni, jamaa ya Wasifoni; wa Hagi, jamaa ya Wahagi; wa Shuni, jamaa ya Washuni;

16. wa Ezboni, jamaa ya Waezboni; wa Eri, jamaa ya Waeri;

17. wa Arodi, jamaa ya Waarodi; wa Areli, jamaa ya Waareli.

18. Hizi ndizo jamaa za wana wa Gadi kama waliohesabiwa kwao, arobaini elfu na mia tano.

19. Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani.

20. Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera.

Hes. 26