Hes. 24:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi Balaamu alipoona ya kuwa ilimpendeza BWANA kuwabariki Israeli, hakwenda, kama hapo kwanza, ili kutafuta uchawi, bali alielekeza uso wake jangwani.

2. Balaamu akainua macho yake akawaona Israeli wamekaa kabila kabila; roho ya Mungu ikamjia.

3. Akatunga mithali yake, akasema,Balaamu mwana wa Beori asema,Yule mtu aliyefumbwa macho asema;

Hes. 24