25. Uwatwae Haruni na mwanawe Eleazari uwalete juu ya mlima wa Hori;
26. umvue Haruni mavazi yake, ukamvike Eleazari mwanawe mavazi hayo; kisha Haruni atakusanywa kwa watu wake, naye atakufa huko.
27. Musa akafanya kama BWANA alivyomwagiza; wakakwea katika mlima wa Hori mbele ya macho ya mkutano wote.
28. Kisha Musa akamvua Haruni mavazi yake, akamvika mwanawe Eleazari mavazi hayo; Haruni akafa huko katika kilele cha mlima; Musa na Eleazari wakatelemka mlimani.
29. Na mkutano wote ulipoona ya kuwa Haruni amekufa, wakamwombolea Haruni muda wa siku thelathini, maana, nyumba yote ya Israeli ikamwombolea.