Hes. 17:7-11 Swahili Union Version (SUV)

7. Kisha Musa akaziweka hizo fimbo mbele za BWANA katika hema ya kukutania.

8. Ilikuwa siku ya pili yake, Musa akaingia ndani ya hema ya ushahidi; na tazama, ile fimbo ya Haruni iliyokuwa kwa nyumba ya Lawi ilikuwa imechipuka, imetoa michipukizi, na kuchanua maua; na kuzaa malozi mabivu.

9. Kisha Musa akazileta nje hizo fimbo zote kutoka hapo mbele za BWANA na kuziweka mbele ya wana wa Israeli wote; nao wakaangalia, na kila mtu akaitwaa fimbo yake.

10. Kisha BWANA akamwambia Musa, Irudishe fimbo ya Haruni mbele ya ushahidi, ili itunzwe iwe ishara juu ya hawa wana wa maasi; ili uyakomeshe manung’uniko yao waliyoninung’unikia, ili wasife.

11. Basi Musa akafanya vivyo; kama BWANA alivyomwagiza, ndivyo alivyofanya.

Hes. 17