Hes. 17:5-7 Swahili Union Version (SUV)

5. Kisha itakuwa, mtu huyo nitakayemchagua, fimbo yake itachipuka; nami nitayakomesha kwangu manung’uniko ya wana wa Israeli, wanung’unikiayo juu yenu.

6. Basi Musa akawaambia wana wa Israeli, ndipo wakuu wao wote wakampa fimbo, fimbo moja kwa kila mkuu, kama nyumba za baba zao zilivyokuwa, fimbo kumi na mbili; na fimbo ya Haruni ilikuwa kati ya fimbo zao.

7. Kisha Musa akaziweka hizo fimbo mbele za BWANA katika hema ya kukutania.

Hes. 17