1. Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,
2. Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli; katika kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja, kila mtu na awe mkuu kati yao.
3. Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na BWANA; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli.
4. Na majina yao ni haya; katika kabila ya Reubeni, Shamua mwana Zakuri.
5. Katika kabila ya Simeoni, Shafati mwana wa Hori.