6. Wa Simeoni; Shelumieli mwana wa Suri-shadai.
7. Wa Yuda; Nashoni mwana wa Aminadabu.
8. Wa Isakari; Nethaneli mwana wa Suari.
9. Wa Zabuloni; Eliabu mwana wa Heloni.
10. Katika wana wa Yusufu; wa Efraimu, Elishama mwana wa Amihudi; na wa Manase; Gamalieli mwana wa Pedasuri.
11. Wa Benyamini Abidani mwana wa Gideoni.
12. Wa Dani; Ahiezeri mwana wa Amishadai.
13. Wa Asheri; Pagieli mwana wa Okirani.
14. Wa Gadi; Eliasafu mwana wa Deueli.
15. Wa Naftali; Ahira mwana wa Enani.
16. Hao ndio walioitwa wa mkutano, wakuu wa kabila za baba zao; nao ndio vichwa vya wale maelfu ya Israeli.