Gal. 6:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.

2. Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.

3. Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake.

Gal. 6