Eze. 45:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Tena, mtakapoigawanya nchi kwa kura iwe urithi, mtamtolea BWANA toleo, sehemu takatifu ya nchi, urefu wake utakuwa urefu wa mianzi ishirini na tano elfu, na upana wake elfu kumi; itakuwa takatifu ndani ya mipaka yake yote pande zote.

2. Katika hiyo itakuwako sehemu kwa mahali patakatifu, urefu wake mia tano, na upana wake mia tano, mraba pande zote; na dhiraa ishirini kwa viunga vyake pande zote.

3. Na kwa kipimo hicho utapima, urefu wa ishirini na tano elfu, na upana wa elfu kumi; na ndani yake patakuwa patakatifu, palipo patakatifu sana.

4. Hiyo ni sehemu takatifu ya nchi; itakuwa ya makuhani, wahudumu wa patakatifu, wakaribiao kumhudumia BWANA; nayo itakuwa mahali kwa nyumba zao, na patakatifu kwa mahali patakatifu.

5. Tena urefu wa ishirini na tano elfu, na upana wa elfu kumi, ni sehemu ya Walawi, wahudumu wa nyumba, iwe milki yao wenyewe kwa vyumba ishirini.

6. Nanyi mtaiandika milki ya mji, upana wake elfu tano, na urefu wake ishirini na tano elfu, kandokando ya mahali palipotolewa, iwe sehemu takatifu; nayo itakuwa ya nyumba yote ya Israeli.

Eze. 45