Eze. 27:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Neno la BWANA likanijia tena, kusema,

2. Na wewe, mwanadamu, mfanyie Tiro maombolezo;

3. umwambie Tiro, Ewe ukaaye penye maingilio ya bahari, uliye mchuuzi wa watu wa kabila nyingi, mpaka visiwa vingi, Bwana MUNGU asema hivi; Wewe, Tiro, umesema, Mimi ni ukamilifu wa uzuri.

Eze. 27