Eze. 23:30-32 Swahili Union Version (SUV)

30. Utatendwa mambo hayo kwa sababu umezini na hao wasioamini, na kwa sababu umetiwa unajisi kwa vinyago vyao.

31. Umekwenda katika njia ya umbu lako; basi nitatia kikombe chake katika mkono wako.

32. Bwana MUNGU asema hivi; Utakinywea kikombe cha umbu lako; chenye nafasi nyingi kikubwa; utadhihakiwa na kudharauliwa; kimejaa sana.

Eze. 23