4. Tazama, watupwa motoni kwa kuni moto umeziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea katikati, je! Wafaa kwa kazi yo yote?
5. Tazama, ulipokuwa mzima, haukufaa kwa kazi yo yote; sembuse ukiisha kuliwa na moto, na kuteketea; je! Waweza kufaa kwa kazi yo yote?
6. Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kama mzabibu kati ya miti ya msituni, niliyoupa moto uwe kuni, ndivyo nitakavyowatoa wakaao Yerusalemu.
7. Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao.
8. Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, kwa sababu wamekosa, asema Bwana MUNGU.