Eze. 13:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Kisha neno la BWANA likanijia, kusema,

2. Mwanadamu, tabiri juu ya manabii wa Israeli wanaotabiri, uwaambie wanaotabiri kwa mioyo yao wenyewe, Lisikieni neno la BWANA;

3. Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao manabii wajinga, wanaoifuata roho yao wenyewe, wala hawakuona neno lo lote!

4. Ee Israeli, manabii wako wamekuwa kama mbweha, mahali palipo ukiwa.

5. Hamkupanda kwenda mahali palipobomolewa, wala hamkuitengenezea nyumba ya Israeli boma, wapate kusimama vitani katika siku ya BWANA.

6. Wameona ubatili, na uganga wa uongo, hao wasemao, BWANA asema; lakini BWANA hakuwatuma; nao wamewatumainisha watu ya kuwa neno lile litatimizwa.

Eze. 13