1. Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
2. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
3. Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.
4. Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.
5. Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;