Ebr. 9:21-23 Swahili Union Version (SUV)

21. Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo.

22. Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.

23. Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.

Ebr. 9