Ebr. 12:3-8 Swahili Union Version (SUV)

3. Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.

4. Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;

5. tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana,Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana,Wala usizimie moyo ukikemewa naye;

6. Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi,Naye humpiga kila mwana amkubaliye.

7. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?

8. Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.

Ebr. 12