Ebr. 1:11-14 Swahili Union Version (SUV)

11. Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu;Nazo zote zitachakaa kama nguo,

12. Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika;Lakini wewe u yeye yule,Na miaka yako haitakoma.

13. Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote,Uketi mkono wangu wa kuumeHata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

14. Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

Ebr. 1