3. Ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu,Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha.
4. Hapo nilalapo chini, nasema,Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu;Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke.
5. Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo;Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena.
6. Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia,Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.
7. Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo;Jicho langu halitaona mema tena.
8. Jicho lake huyo anionaye halitaniangalia tena;Macho yako yatanielekea, lakini sitakuwapo.
9. Kama vile wingu likomavyo na kutoweka,Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.