17. Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye;Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi.
18. Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza;Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya.
19. Yeye atakuokoa na mateso sita;Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa.
20. Wakati wa njaa atakukomboa na mauti;Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga.
21. Utafichwa na mapigo ya ulimi;Wala usiogope maangamizo yatakapokuja.
22. Wewe utayacheka maangamizo na njaa;Wala hutawaogopa wanyama wakali wa nchi.
23. Kwani utakuwa na mapatano na mawe ya bara;Nao wanyama wa bara watakuwa na amani kwako.
24. Nawe utajua ya kwamba hema yako ina salama;Na zizi lako utaliaua, wala usikose kitu.
25. Tena utajua ya kwamba uzao wako utakuwa mwingi,Na vizazi vyako watakuwa kama nyasi za nchi.