Ayu. 41:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana?Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?

2. Je! Waweza kutia kamba puani mwake?Au kutoboa taya yake kwa kulabu?

3. Je! Atakusihi sana?Au, atakuambia maneno ya upole?

4. Je! Atafanya agano pamoja nawe,Umtwae kuwa mtumishi wako milele?

Ayu. 41