Ayu. 4:9-15 Swahili Union Version (SUV)

9. Kwa pumzi za Mungu huangamia.Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika.

10. Kunguruma kwake simba, na sauti ya simba mkali,Na meno ya simba wachanga, yamevunjika.

11. Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo,Nao watoto wa simba mke wametawanyika mbalimbali.

12. Basi, nililetewa neno kwa siri,Sikio langu likasikia manong’ono yake.

13. Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku,Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.

14. Hofu iliniangukia na kutetema,Iliyoitetemesha mifupa yangu yote.

15. Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu;Na nywele za mwili wangu zilisimama.

Ayu. 4