Ayu. 4:15-21 Swahili Union Version (SUV)

15. Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu;Na nywele za mwili wangu zilisimama.

16. Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake,Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu;Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,

17. Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu?Je! Mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake?

18. Tazama, yeye hawategemei watumishi wake;Na malaika zake huwahesabia upuzi;

19. Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo,Ambazo misingi yao i katika mchanga,Hao waliosetwa mbele ya nondo!

20. Kati ya asubuhi na jioni huvunjwa-vunjwa;Waangamia milele wala hapana atiaye moyoni.

21. Je! Kamba ya hema yao haikung’olewa ndani yao?Wafa, kisha hali hawana akili.

Ayu. 4