Ayu. 38:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,

2. Ni nani huyu atiaye mashauri gizaKwa maneno yasiyo na maarifa?

3. Basi jifunge viuno kama mwanamume,Maana nitakuuliza neno, nawe niambie.

4. Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.

5. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua?Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?

6. Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,

Ayu. 38