17. Lakini umejaa hukumu ya waovu;Hukumu na haki hukushika.
18. Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha;Wala usikubali ukuu wa ukombozi ukugeuze.
19. Je! Mali yako yatatosha, hata usiwe katika taabu,Au uwezo wote wa nguvu zako?
20. Usiutamani usiku,Wakati watu wakatwapo katika mahali pao.
21. Jitunze, usiutazame uovu;Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu.
22. Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake;Ni nani afundishaye kama yeye?
23. Ni nani aliyemwagiza njia yake?Au ni nani awezaye kusema, Wewe umetenda yasiyo haki?
24. Kumbuka kuitukuza kazi yake,Watu waliyoiimbia.
25. Wanadamu wote wameitazama;Watu huiangalia kwa mbali
26. Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui;Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
27. Kwani yeye huvuta juu matone ya maji,Yamwagikayo katika mvua kutoka kungeni mwake;
28. Ambayo mawingu yainyeshaNa kudondoza juu ya wanadamu kwa wingi.
29. Naam, mtu aweza kuelewa na matandazo ya mawingu,Ngurumo za makao yake?
30. Tazama, yeye huutandaza mwanga wake, umzunguke;Naye hufunika vilindi vya bahari.
31. Kwani huwahukumu kabila za watu kwa njia hizi;Hutoa chakula kwa ukarimu.
32. Yeye huifunika mikono yake kwa umeme;Na kuuagiza shabaha utakayopiga.
33. Mshindo wake hutoa habari zake,Anayewaka hasira juu ya uovu.