1. Tena Elihu akaendelea na kusema,
2. Ningojee kidogo nami nitakueleza;Kwa kuwa nikali na maneno kwa ajili ya Mungu.
3. Nitayaleta maarifa yangu kutoka mbali,Nami nitampa haki Muumba wangu.
4. Kwani yakini maneno yangu si ya uongo;Aliyekamilika katika maarifa yu pamoja nawe.
5. Tazama, Mungu ni hodari, wala hamdharau mtu ye yote;Ana uweza katika nguvu za fahamu.
6. Hauhifadhi uhai wa waovu;Lakini huwapa wateswao haki yao.
7. Yeye hawaondolei macho yake wenye haki;Lakini pamoja na wafalme huwawekaKatika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.