1. Tena Elihu akajibu na kusema,
2. Je! Wewe wadhani kwamba haya ni haki yako,Au je! Wasema, Haki yangu ni zaidi kuliko ya Mungu,
3. Maana wasema, Kutakuwa na faida gani kwako wewe?Tena, Nitapata faida gani, kuliko nikifanya dhambi?
4. Mimi nitakujibu,Na hawa wenzio pamoja nawe.