12. Naam, hakika, Mungu hatatenda mabaya,Wala Mwenyezi hatapotosha hukumu.
13. Ni nani aliyemwagiza kuiangalia dunia?Au ni nani aliyemwekea ulimwengu huu wote?
14. Kama akimwekea mtu moyo wake,Akijikusanyia roho yake na pumzi zake;
15. Wenye mwili wote wataangamia pamoja,Nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi.
16. Ikiwa una ufahamu, sikia neno hili;Isikilize sauti ya maneno yangu.
17. Je! Atatawala mtu aichukiaye haki hata mmoja?Nawe, je! Utamhukumia mkosa aliye na haki na mwenye nguvu?