Ayu. 31:4-11 Swahili Union Version (SUV)

4. Je! Yeye hazioni njia zangu,Na kuzihesabu hatua zangu zote?

5. Kwamba nimetembea katika ubatili,Na mguu wangu umeukimbilia udanganyifu;

6. (Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa,Ili Mungu aujue uelekevu wangu);

7. Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia,Na moyo wangu kuyaandama macho yangu,Tena kwamba kipaku cho chote kimeshikamana na mikono yangu;

8. Basi na nipande, mwingine ale;Naam, mazao ya shamba langu na yang’olewe.

9. Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke,Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu;

10. Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine,Na wengine na wainame juu yake.

11. Kwani hilo lingekuwa kosa kuu;Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;

Ayu. 31