1. Nilifanya agano na macho yangu;Basi nawezaje kumwangalia msichana?
2. Kwani sehemu ya Mungu itokayo juu ingekuwa nini,Na urithi wa Mwenyezi utokao juu?
3. Je! Siyo msiba kwa wasio haki,Na hasara kwao watendao uovu?
4. Je! Yeye hazioni njia zangu,Na kuzihesabu hatua zangu zote?