Ayu. 24:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Mbona nyakati zisiwekwe na Mwenyezi?Na hao wamjuao mbona hawazioni siku zake?

2. Wako waziondoao alama za mipaka;Huyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.

3. Humfukuza punda wake asiye baba,Humtwaa rehani ng’ombe wake mwanamke mjane.

4. Humgeuza mhitaji aiache njia;Maskini wa nchi hujificha pamoja.

5. Tazama, kama punda-mwitu jangwaniWao hutoka kwenda kazini mwao, wakitafuta chakula kwa bidii;Jangwa huwapa chakula cha watoto wao.

6. Hukata nafaka zao mashambani;Na kuokota zabibu za waovu.

7. Hujilaza usiku kucha uchi pasipo nguo,Wala hawana cha kujifunika baridi.

8. Hutota kwa manyunyo ya milimani,Na kuambatana na jabali kwa kukosa sitara,

Ayu. 24