5. Ningeyajua maneno atakayonijibu,Na kuelewa na hayo atakayoniambia.
6. Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake?La, lakini angenisikiliza.
7. Hapo walekevu wangepata kuhojiana naye;Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele.
8. Tazama, naenda mbele, wala hayuko;Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;
9. Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona;Hujificha upande wa kuume, hata nisimwone.
10. Lakini yeye aijua njia niendeayo;Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
11. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake;Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.