Ayu. 22:27-30 Swahili Union Version (SUV)

27. Utamwomba yeye naye atakusikia;Nawe utazitimiliza nadhiri zako.

28. Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako;Na mwanga utaziangazia njia zako.

29. Hapo watakapokuangusha, utasema, Kuna kuinuka tena;Naye mnyenyekevu Mungu atamwokoa.

30. Atamwokoa na huyo asiye na hatia;Naam, utaokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako.

Ayu. 22