18. Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema;Lakini mashauri ya waovu na yawe mbali nami.
19. Wenye haki huyaona hayo wakafurahi;Nao wasio na hatia huwacheka;
20. Wasema, Hakika hao waliotuinukia wamekatiliwa mbali,Na mabaki yao moto umeyateketeza.
21. Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;Ndivyo mema yatakavyokujia.
22. Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake,Na maneno yake yaweke moyoni mwako.
23. Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa;Ukiuondoa udhalimu mbali na hema yako.