13. Nawe wasema, Mungu anajua nini?Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu?
14. Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione;Naye yuatembea juu ya kuba ya mbingu.
15. Je! Utaiandama njia ya zamaniWaliyoikanyaga watu waovu?
16. Ambao walinyakuliwa kabla ya wakati wao,Msingi wao ulimwagika kama kijito cha maji;
17. Waliomwambia Mungu, Tuondokee;Tena, Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?
18. Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema;Lakini mashauri ya waovu na yawe mbali nami.
19. Wenye haki huyaona hayo wakafurahi;Nao wasio na hatia huwacheka;
20. Wasema, Hakika hao waliotuinukia wamekatiliwa mbali,Na mabaki yao moto umeyateketeza.
21. Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;Ndivyo mema yatakavyokujia.
22. Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake,Na maneno yake yaweke moyoni mwako.