1. Roho yangu imezimika, siku zangu zimekoma,Kaburi i tayari kunipokea.
2. Ni kweli wako kwangu wenye kufanya dhihaka,Jicho langu hukaa katika kunifanyia uchungu kwao.
3. Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe;Kuna nani atakayeniwekea dhamana?