Ayu. 16:9-13 Swahili Union Version (SUV)

9. Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea;Amesaga-saga meno juu yangu;Mtesi wangu hunikazia macho makali.

10. Wamenifumbulia vinywa vyao;Wamenipiga shavuni kwa kunitukana;Hujikutanisha pamoja juu yangu.

11. Mungu amenitia kwa hao wapotovu,Na kunitupa mikononi mwao waovu.

12. Nilikuwa katika raha, naye akanivunja-vunja;Naam, amenishika shingo, na kuniponda;Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.

13. Wapigaji wake wa mishale hunizingira kotekote,Hunipasua viuno vyangu, asinihurumie;Nyonga zangu amezimwaga juu ya nchi.

Ayu. 16