5. Lakini ningewatia nguvu kwa kinywa changu,Na utuzo wa midomo yangu ungetuliza.
6. Nijapokuwa nanena, huzuni yangu haitulizwi;Nijapokuwa najizuia, nimepunguziwa kitu gani?
7. Lakini sasa amenichokesha;Jamii yangu yote umeifanya ukiwa.
8. Umenishika sana, ni ushahidi juu yangu;Na kukonda kwangu kwaniinukia, kwanishuhudia usoni pangu.
9. Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea;Amesaga-saga meno juu yangu;Mtesi wangu hunikazia macho makali.
10. Wamenifumbulia vinywa vyao;Wamenipiga shavuni kwa kunitukana;Hujikutanisha pamoja juu yangu.
11. Mungu amenitia kwa hao wapotovu,Na kunitupa mikononi mwao waovu.