21. Sauti za utisho zi masikioni mwake;Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake;
22. Yeye hasadiki kwamba atarudi kutoka gizani,Naye hungojewa na upanga;
23. Hutanga-tanga ili apate chakula, akisema, Ki wapi?Ajua kwamba siku ya giza i tayari karibu yake;
24. Mateso na dhiki humtia hofu;Humshinda kama vile mfalme aliye tayari kwa vita;
25. Kwa kuwa amenyosha mkono wake juu ya Mungu,Na kuendelea kwa kiburi kinyume cha Mwenyezi;
26. Humshambulia na shingo ngumu,Kwa mafundo makubwa ya ngao zake;