Ayu. 12:6-13 Swahili Union Version (SUV)

6. Hema za wapokonyi hufanikiwa,Na hao wamkasirishao Mungu hukaa salama;Mikononi mwao Mungu huleta vitu vingi.

7. Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha;Na nyuni wa angani, nao watakuambia;

8. Au nena na nchi, nayo itakufundisha;Nao samaki wa baharini watakutangazia.

9. Katika hawa wote ni yupi asiyejua,Kwamba ni mkono wa BWANA uliofanya haya?

10. Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake,Na pumzi zao wanadamu wote.

11. Je! Sikio silo lijaribulo maneno,Kama vile kaakaa lionjavyo chakula?

12. Wazee ndio walio na hekima,Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu.

13. Hekima na amri zina yeye [Mungu];Yeye anayo mashauri na fahamu.

Ayu. 12